27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Dayna Nyange ahadi kibao 2016

daynaNA THERESIA GASPER

BAADA ya kimya kirefu katika muziki wa kizazi kipya, Dayna Nyange ameibuka na kutangaza kurudi upya kwa ‘surprise’ ya wimbo mpya na mipango mipya katika mwaka huu.

Dayna alisema mwaka uliopita alishindwa kwenda na wakati, ndiyo maana hakufanya vizuri sana, lakini mwaka huu amejipanga kwenda na kasi ya muziki, huku akidai wimbo anaotaraji kuuachia ni ‘surprise’ kwa mashabiki wake.

“Mashabiki wangu wamekosa vitu vingi, ikiwemo shoo zangu za nguvu, nyimbo zangu za mahaba na makeke yangu niwapo jukwaani, lakini wasiwe na hofu, kwa kuwa nimerudi upya kuwatetea kiburudani,’’ alijinadi Dayna.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles