24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Lupita naye azikosoa tuzo za Oscar

Lupita Nyong'oNEW YORK, MAREKANI

MSHINDI wa tuzo ya Oscar mwaka 2014 kupitia filamu ya ‘Twelve Years a Slave’ ambaye ni raia wa Kenya anayeishi nchini Marekani, Lupita Nyong’o, ameungana na wacheza filamu wengine kuwashutumu waandaaji wa tuzo za Oscar kwa kufanya ubaguzi wa rangi.

Waandaaji wa tuzo hizo mwaka huu wameonyesha wazi ubaguzi ambapo wamewaweka watu weupe katika kuwania tuzo hizo, huku weusi wakiwa katika ugawaji badala ya kuwania tuzo hizo.

Katika akaunti yake ya Istagram, Lupita ameandika kwamba amekasirishwa na namna ambavyo watu weusi hawajajumlishwa katika tuzo hizo, badala yake kupewa nafasi ya kuwa wagawaji wa tuzo hizo kwa watu weupe.

“Ni jambo la kusikitisha sana kuona tuzo hizo mwaka huu zinawapa watu weupe wakati wapo weusi wanaofanya vizuri na wanastahili kutwaa, huu ni ubaguzi wa rangi na haina maana yoyote,” aliandika Lupita.

Mwaka 2014 Lupita alishinda tuzo hiyo kutokana na uwezo wake ambao aliuonesha katika filamu ya Twelve Years a Slave.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles