25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

DAWASA waingia mtaani kubadili mita za maji

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeanza zoezi la kufanya ubadilishaji wa dira za maji za wateja kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji huduma.

Zoezi la ubadilishaji wa dira za maji limeanza kutekelezwa mapema mwezi Februari na linahusisha mikoa yote 22 ya kihuduma na litahusisha ubadilishaji wa mita za maji zilizoharibika, zenye umri mkubwa (zaidi ya miaka mitano) zilizosimama, na mita chakavu.

Akizungumzia zoezi hilo leo Februari 5, kwa eneo la Tegeta Mhandisi wa Dawasa Tegeta, Dominick Mkamba, amesema zoezi la kubadilisha dira za maji linalenga kuongeza ufanisi na kuepusha adha zitokanazo na uwepo wa mita mbovu zinazoleta hasara kwa mamlaka na wateja pia.

“Zoezi la kubadilisha mita za maji linahususha mita zote zilizosimama, zilizopoteza ufanisi kwa maana ya kutokuonekana vizuri, mita za muda mrefu na mita zilizoshindwa kutengemaa,” amesema Mhandisi Mkamba.

Kwa upande wa Temeke Mhandisi wa DAWASA Temeke, Ramadhani Sangali, amesema zoezi la ubadilishaji mita za wateja linaenda sambamba na zoezi la kubadilisha mabomba chakavu ya maji kwa eneo la Temeke.

“Mkoa wetu wa Temeke tumejipanga kubadilisha mita za maji takribani 900 ambazo ni mita chakavu, mbovu, zilizosimama na zile zilizopo muda mrefu kwa wateja, na sasa tumeanza ubadilishaji huo eneo la Keko na tunaendelea kwa maeneo yote ndani ya eneo letu la kihuduma Temeke,” amesema Mhandisi Sangali.

Zoezi la ubadilishaji mita za maji ni zoezi endelevu na linalofanywa na Mamlaka likiwa na lengo la kuongeza mauzo ya maji, kuongeza makusanyo na kupunguza malalamiko ya wateja juu ya ankara.

Zoezi la ubadilishaji wa mita za maji hufuata taratibu zifuatazo;
. Kuzitambua mita za muda mrefu na zisizo na ufanisi
. Taarifa ya mita mbovu kutolewa taarifa katika kitengo cha mita
. Kumshirikisha mteja juu ya ubadilishaji mita yake kwa kumpa elimu
. Kujaza fomu maalumu ya kubadilisha mita, fomu itajazwa na msimamizi kitengo cha mita na kuwekwa sahihi na mteja
. Fomu kurudishwa kwa Afisa Ankara kwa ajili ya kubadilisha maelezo kwenye mfumo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles