24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

DAWA YA VVU KUTOLEWA KWA SINDANO

PARIS, UFARANSA


MATIBABU dhidi ya virusi vya Ukimwi (VVU) yanatarajiwa kutolewa kupitia sindano.

Kwa mujibu wa wanasayansi, dawa hiyo itakuwa ikitolewa mara sita kwa mwaka.

Wamesema kuwa kubuniwa kwa muundo huo mpya wa dawa ya VVU kutolewa kwa sindano, kunaweza kutoa tiba fanisi zaidi iwapo itapitishwa.

Tiba hiyo ya sindano, ambayo huendelea kuingiza taratibu dawa ya VVU katika damu ya mgojwa, iko katika hatua ya pili ya majaribio.

Dawa hiyo inatarajiwa kupunguza mzigo wa dozi za vidonge na kutoa ahueni kwa watu wanaoishi na VVU mara itakapopitishwa.

Watu wengi huhangaika kumeza dawa kila siku na katika kesi nyingi husababisha VVU kurudi na kuwapo usugu dhidi ya dawa.

Matokeo hayo yaliwasilishwa juzi Jumanne katika Mkutano wa Kimataifa wa Ukimwi kuhusu sayansi ya VVU mjini Paris, Ufaransa.

“Kama utafiti wa dawa mpya ya kukabiliana na VVU, kufuata masharti ya tiba kunaendelea kuwa njia nzuri zaidi ya kukabili VVU na kupunguza usugu dhidi ya dawa,” alisema Dk. David Margolis, mtafiti kutoka taasisi ya ViiV Healthcare.

Katika matokeo ya utafiti, kulikuwa na asilimia 94 ya kukabili virusi kwa wagonjwa waliowekewa mseto wa dawa mbili kila baada ya wiki nane. Wiki nne ziliripoti ufanisi wa asilimia 87 kulinganisha na asilimia 84 kwa wagonjwa waliotumia mseto wa dawa ya kumeza.

“Hakukuwa na wagonjwa walioashiria kuwapo usugu wa VVU dhidi ya dawa, maumivu kutokana na sindano ndiyo yaliyoripotiwa zaidi.

“Athari za dawa ikiwamo kuhara na maumivu ya kichwa, yalishuhudiwa katika makundi yote,” alisema.

Utafiti mwingine ulihitimisha kwamba uanzishaji wa kinga za mwili kwa watu walioathirika kunaweza kuchelewesha kuzaliana kwa VVU mwilini, hasa baada ya kuvurugwa kwa tiba ya dawa za kumeza za kufubaza makali ya VVU (ARVs).

Utafiti unaojulikana kama RV397 ulitaka kupata matibabu ambayo yanaweza kuzuia mizigo ya virusi bila ya haja ya kutumia ARVs kila siku.

Wanasayansi walijaribu kuangalia athari za kinga za mwili za VRCO1  ili kutambua mabadilikio ya virusi kwa watu walioathirika na VVU na ambao wamekuwa katika tiba ya ARVs.

VRCO1 ni kinga ya mwili, ambayo inazuia mashambulizi mengi yanayosababishwa na VVU.

“Hiyo ni mara ya kwanza kwa kinga ya VRCO1 kutathminiwa kwa watu, ambao walianza dawa wakati wa maambukizo makali ya VVU,” alisema Dk. Trevor Crowell, aliyewasilisha utafiti huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles