27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

RUTO ADAI RAILA NI MCHAWI

NAIROBI, KENYA


MAKAMU wa Rais wa Kenya, William Ruto, amemshambulia mgombea urais wa NASA, Raila Odinga kuwa ni mchawi.

Akizungumza Kuresoi Kusini, Naibu Rais Ruto alikuwa akirejea kitendo cha mwanasiasa kutoka jamii yake ya Kalenjin, Isaac Ruto kujiunga na NASA.

Ruto alidai kuwa Isaac Ruto ambaye pia ni gavana wa Kaunti ya Bomet, alikuwa alidhibitiwa na nguvu za giza za Raila.

“Yamkini Gavana Ruto amerogwa na Raila. Nimejaribu mara kadha kuzungumza naye, lakini acha aendelee jinsi alivyo,” alisema Ruto.

Pia alimtaja Raila kama mnyanyasaji ambaye hana rekodi yoyote ya maendeleo ya kuwapa wapigakura 949,618 waliosajiliwa Kaunti ya Nakuru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles