26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 30, 2024

Contact us: [email protected]

Dar yajipanga kuendelea kuongoza matokeo darasa la saba

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeweka mikakati ya kuhakikisha inaendelea kubaki kileleni katika matokeo ya darasa la saba.

Katika matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2021 Dar es Salaam iliongoza kitaifa kwa ufaulu wa asilimia 96.54 huku Ilala CC ikiongoza kwa asilimia 98.52 na Ilala asilimia 96.28.

Ofisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Sipora Tenga, akimpongeza Ofisa Elimu Msingi mstaafu wa halmashauri hiyo, Elizabeth Thomas, kwa kutambua mchango wake katika idara hiyo.

Akizungumza wakati wa halfa ya kupongezana na kuwapa tuzo viongozi wa dara ya elimu msingi katika vitengo mbalimbali Ofisa Elimu Msingi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Tenga, amesema siri ya mafanikio hayo ni ushirikiano na utiifu wa walimu waliopo katika halmashauri hiyo.

“Siri ya mafanikio ni umoja wetu na ushirikiano, tuna umoja wa walimu wakuu na viongozi idara ya elimu na maofisa elimu wa kata. Tumejipanga tuna kata 36 tuna viongozi wa Klasta ambazo zinasaidia kuhakikisha tunapofanya mtihani ni maswali gani wanafunzi walishindwa.

“Tumeshirikiana katika kupata ufaulu mzuri na tunajipanga vizuri kuhakikisha nafasi tuliyoipata tunaendelea kuishikilia, najua ushindani ni mkubwa lakini tumejipanga vizuri,” amesema Mwalimu Sipora.

Ofisa huyo amewataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wao na kuhakikisha watoto wanakwenda shule wakiwa na mahitaji yote muhimu sambamba na kuwapatia chakula ili waweze kusoma vizuri.

Naye Ofisa Elimu Msingi mstaafu wa halmashauri hiyo, Elizabeth Thomas ambaye alikuwa mgeni rasmi, ameipongeza halmashauri hiyo na kuwataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili waweze kufanikiwa.

“Nina furaha kwa sababu hamkumuangusha mama Tenga na mimi hamkuniangusha, mmefanya kazi nzuri nategemea mwaka huu mtaendeleza rekodi nzuri ya ufaulu,” amesema Elizabeth.

Katika hafla hiyo watumishi kutoka idara ya elimu msingi kitengo cha taaluma, vifaaa na takwimu, elimu ya watu wazima, masijala, maktaba na utamaduni na michezo walikabidhiwa tuzo kutambua mchango wao uliowezesha halmashauri hiyo kufanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles