DABA waja na mashindano ya majaribio

0
693

Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam

Chama cha Ngumi za Ridhaa mkoa wa Dar es Salaam (DABA) umeandaa mashindano ya majaribio ambayo yamepangwa kufanyika Machi 20 mwaka huu kwenye Ukumbi wa CCM Amana, Ilala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na www.mtanzania.co.tz Mwenyekiti wa DABA, Akalory Godfrey, amesema yatashirikisha vilabu mbalimbali jijini .

Amesema lengo ni kuwaandaa na kuwaweka tayari mabondia kushiriki mashindano ya wazi wa mkoa wa Dar es salaam yatakayoanza Aprili 7 hadi 10 jijini humo.

“Kabla ya kuelekea kwenye mashindano ya mkoa, tutaanza mashindano ya majaribio ambayo yatakuwa ni kipimo cha Makocha wa vilabu kuimarisha wachezaji wawe na ushindani,” amesema Godfrey.

Ametoa wito kwa vilabu kujitokeza kwa wingi kushiriki mashindano hayo ya majaribio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here