25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Gold Land Kigamboni hakuna mbabe

Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam

Timu ya Gold Land imetoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya Kingamboni Soccer katika mchezo wa Ligi ya Vijana chini ya miaka 20 inayoendelea kwenye Uwanja wa Shule ya msingi Kingamboni, Dar es salaam.

Wakizungumza na www.mtanzania.co.tz Makocha wa timu hizo kwa nyakati tofauti tofauti baada ya kuamlizika kwa mchezo huo .

Kocha wa Gold Land, Khatib Ally, amesema mchezo ulikuwa mzuri na ushindani mkubwa.

Ally amesema kuwa wamepokea matokeo ,hivyo watakwenda kujipanga kwa mchezo ujao.

Kwa upande wake kocha wa Kingamboni Soccer Kiiza Yahya,amesema nafasi walipata lakini walishinda kuzitumia.

Amesema pia walishindwa kutimia kasoro za wapinzani wao na kusababisha kutoka suluhu.

“Katika matokeo haya hakuna wa kumlaumu ,hivyo tunakwenda kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza na malengo yetu ni kupata pointi tatu,” amesema Yahya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles