26.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

Ummy awataka Wanawake kufanya makubwa katika jamii

Na Brigther Masaki, Dar es Salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu, amewataka Wanawake kufanya makubwa katika jamii na kuacha kujibweteka huku wakitiana moyo wao kwa wao.

Akizungumza wakati wa kutoa tuzo usiku wa kuamkia leo Machi 10, 2021 jijini Dar es Salaam, zilizoandaliwa na Tanzania Women Industrial Awards, (TWCC) na kutolewa na Waziri Ummy, kwa Wanawake wenye mchango kwenye jamii, amesema ni wakati wa wanawake kuwa vinara na kutiana moyo.

“Mwanamke unatakiwa kuwa wakwanza kumtia moyo mwenzako katika safari anayoinza iwe ya biashara au ya uongozi ndio chachu ya yeye kutimiza malengo yake hata Mimi nilipoanza kuna watu walinitia moyo ambao wamesababisha leo kuwa Waziri,” amesema Ummy.

Miongoni mwa watu waliopata tuzo hizo ni pamoja na Mbunifu wa Mavazi nchini, Agustar Masaki, AgustarFashion.Tz ambaye amepatia tuzo ya Mwanamitindo bora wa mwaka anayefanya vizuri na kuinua vipaji kwa wabunifu wachanga.

“Namshukuru Mungu na TWCC kwa kuona mchango wangu wa kuinua vipaji vya wabunifu na wanamitindo wachanga kwenye jamii ili kuweza kutimiza ndoto zao,” amesema Agustar.

Naye Msanii mkongwe wa Filamu nchini Natasha Lewis maarufu Mamvi amepata tuzo ya msanii mwanamke mwenye heshima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,348FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles