NYOTA wa kikapu wa timu ya Golden State Warrior, Stephen Curry, anaongoza kwa mauzo ya jezi katika michuano ya Ligi ya NBA nchini Marekani.
Mchezaji huyo bora wa tuzo za MVP msimu uliopita, amekuwa na idadi kubwa ya mashabiki na kuifanya jezi yake kuuzika sana sokoni na kuwafunika nyota wengine kama vile LeBron James wa Cleveland Cavaliers na Kobe Bryant wa Los Angeles Lakers.
Mchezaji huyo amefamnya mauzo makubwa kwa miezi mitatu tangu Oktoba 2015 hadi Desemba mwaka huo huo.
James na Bryant, ambao wanatarajia kustaafu kikapu mwishoni mwa msimu huu, wamekuwa nafasi ya pili na tatu kwa mauzo, wakati nyota wa timu ya New York Knicks, Kristaps Porzingis akishika nafasi ya nne.
Kevin Durant, Derrick Rose, Russell Westbrook, Kyrie Irving, James Harden na Jimmy Butler wameingia katika nafasi 10 za majina yao kuuzika katika jezi.