23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

CUF yapata Naibu Meya Dar

Mussa Swedi KafanaNA MAULI MUYENJWA, DAR ES SALAAM

DIWANI wa kata ya Kiwalani, Mussa Kafana (CUF), amechaguliwa kuwa Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, baada kumshinda mpinzani wake, Mariam Lulida (CCM).

Uchaguzi huo ulifanyika jana katika kikao cha kwanza cha Baraza la Jiji la Dar es Salaam kilichofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee.

Kafana ambaye chama kipo katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), aliibuka mshindi baada ya kupata kura 10 dhidi ya sita alizopata Mariam.

Uchaguzi huo umekamilika baada ya mchakato mrefu wa kumpata Meya wa Jiji,  uliohitimishwa Machi 22, mwaka huu kutokana  na kutawaliwa na mvutano kati ya CCM na Ukawa uliosababisha uahirishwe mara tatu.

Uchaguzi wa jana haukutarajiwa kuwa na mvutano mkubwa kati ya Ukawa na CCM kutokana na idadi ya wapigakura kuwa ndogo kwa kuwa haujumuishi madiwani wote, isipokuwa wajumbe 18.

Kati ya wajumbe hao, kila manispaa ilitoa wanne wakiwamo mameya wakati wabunge watano wa majimbo waliruhusiwa kuingia kwenye baraza hilo lililokuwa chini ya Meya wa Jiji, Isaya Mwita (Chadema).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles