26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

CUF-Maalim Seif asiachiwe urais mwenyewe

seifNA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimewataka wanachama wake wenye sifa za kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar wajitokeze kuchukua fomu kugombea nafasi hiyo.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho, Omar Ali Shehe, amewaambia waandishi wa habari jana kwamba, wanachama wanatakiwa wasimuachie Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharrif Hamad, kuchukua fomu ya urais peke yake.

“Tunawataka wanachama wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu za kugombea urais, wasimuachie Maalim Seif peke yake ili kuondoa manung’uniko kuwa ndiye anayefaa katika chama.

“Kazi ya kuchukua fomu hizi inaanza kesho (leo) kwa muda wa wiki moja na kumalizika Mei 31, mwaka huu, siku hiyo ndiyo mwisho wa urejeshaji wa fomu hizo zitakazouzwa kwa Sh 500,000 na zitatolewa kwa makatibu wa wilaya,” alisema Shehe.
Alisema pamoja na mambo mengine, chama hicho kimekubaliana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwa mgombea urais upande wa Zanzibar atakayesimama atatoka CUF.
Alisema katika Jimbo la Kikwajuni, kwa nafasi ya ubunge watasimamisha mgombea kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Alisema baada ya kukamilika uchukuaji na urejeshaji, majina ya wagombea yatapelekwa Kamati Tendaji Taifa ili kupigiwa kura ya maoni.
Baada ya hapo, yatapelekwa Baraza Kuu kwa ajili ya ukaguzi na kutoa uamuzi kama mgombea anafaa au la.

“Hata kama atajitokeza mtu mmoja tu kuchukua fomu ya urais, lazima apitie hatua za mkutano wa Kamati Tendaji kama taratibu zetu zinavyoonyesha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles