26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

CR7 avunja rekodi

JANA Cristiano Ronaldo alifunga mara mbili na kuiwezesha timu ya taifa ya Ureno kushinda mabao 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Ireland katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwakani.

Hivyo, sasa Ronaldo amefikisha mabao 111 na kuipiku rekodi ya mkongwe wa Iran, Ali Daei, ambaye ndiye aliyekuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi (109) akiwa na timu ya taifa.

Wakati huo huo, hatua ya ‘CR7’ kuondoka Juventus imesababisha ugomvi mkubwa kati ya kocha wao, Massimiliano Allegri, na mabosi wa klabu hiyo.

Taarifa zimedai kuwa Allgeri ameonesha hasira zake dhidi ya Rais wa Juve, Andrea Agnelli, sambamba na mkurugenzi wa michezo klabuni hapo, Federico Cherubini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles