26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Chemical: Mimi bado bikira

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Msanii wa kike wa miondoko ya  ‘hip hop’ nchini,  Claudia Lubao maarufu  Chemical, amesema  hajawahi  kukutana na mwanaume kimwili, hivyo bado ni bikira na hadi sasa hana mtu yoyote anayemmiliki.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo, Chemical amesema anafurahi kuwa hivyo na atarajia mume atakayempata atafurahi kwa sababu anajua kupenda, muelewa na hatampangia vigezo vya mahari.

“Mahusiano ni kama unaishi na wazazi, utaulizwa kwa nini umechelewa, ulikuwa wapi kwa hiyo mimi bado nipo ‘single’.

“Chemical ndio msichana pekee Tanzania mwenye hiyo sifa, mtoto bado mbichi, bikira kwani ni tusi? Sijaguswa, mtoto mlaini. Mtu akiamua kunioa nitamtunuku tu, sijaona sababu ya kutoa mahali sababu haitasaidia.

“Kwa ‘future hubby’ wangu namwambia atafurahia sana sababu mimi ni mtu fulani hivi anajua kupendwa anajua kupenda pia. Nikikupenda utafurahi sana,,”amesema Chemical.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles