RIO, Brazil
MASENETA nchini Brazil wamepiga kura ya kutaka Rais Jair Bolsonaro kufunguliwa mashitaka kwa namna alivyoshindwa kuweka mikakati ya kupambana na janga la Corona.
Kwa mujibu wa kile walichokiona maseneta hao, Rasi Bolsonaro anapaswa kufikishwa kwenye mkono wa sheria kwa kosa la kupuuza maisha ya watu baada Corona kuua raia 600,000.
Hata hivyo, hofu ya wengi ni kwamba huenda lisitokee hilo la kufunguliwa mashitaka kwani Mwendesha Mashitaka Mkuu, Augusto Aras, ni miongoni mwa walioteuliwa na Rais huyo.
Mbali ya hoja hiyo ya uhalifu dhidi ya binadamu, Kamati ya Maseneta imependekeza mashitaka mengine nane dhidi ya kiongozi huyo, likiwamo la kughushi nyaraka zilizotumika kueneza taarifa zisizo sahii juu ya Corona.