27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 7, 2023

Contact us: [email protected]

Jeshi Sudan: Tumepindua Serikali kuzuia vita

KHARTOUM, Sudan

JENERALI Abdel Fattah al-Burhan, ambaye hivi karibuni ndiye aliyeongoza mapinduzi ya kuing’oa Serikali iliyokuwa madarakani nchini Sudan, ametetea uamuzi wa hicho walichokifanya.

Kwa mujibu wa Jenerali, waliona wapindue Serikali kwa kuwa vilikuwapo viashiria vya vita ya wenyewe kwa wenyewe ambayo ingetokana na maandamano ya raia yaliyosababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu.

“Hatari iliyoonekana wiki iliyopita ingeweza kuipeleka nchi kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe,” amesema Jenerali Burhan akiwaambia waandishi wa habari jana.

Aidha, amezungumzia hatua ya kumshikilia Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Abdalla Hamdok, akisema walifanya hivyo kwa usalama wake kwani angeweza kudhurika kutokana na maandamano hayo yaliyotajwa kuua watu 10.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles