24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Corona yafunga Hoteli ya Tanga Beach Resort

Mwandishi wetu –Tanga

MENEJIMENTI ya uongozi wa hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Tanga Beach Resort iliyoko jijini Tanga, imelazimika kufunga hoteli hiyo ili kuunga mkono jitihada za Serikali za kuzuia mikusanyiko ili kujikinga na ugonjwa wa corona unaotokisa dunia kwa sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini hapa, Meneja wa hoteli hiyo, Joseph Ngonyo, alisema kuwa wameamua kuifunga kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo hapa nchini pamoja na kudhibiti mikusanyiko ya watu

Alisema kuwa awali tayari biashara ya hoteli ilianza kusuasua kutokana na uwepo wa ugonjwa huo, hivyo kulazimika kufunga ili kuzuia mkusanyiko wa watu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika msimu wa sikukuu.

“Dunia sasa hivi na hata nchini kwetu kumekuwa na tatizo la gonjwa la corona, hivyo tumeamua kusitisha huduma ili kuunga mkono kauli ya Serikali ya kuzuia mkusanyiko wa watu wengi pamoja, hivyo ili kuwadhibiti tumelazimika kufunga hoteli hiyo,” alisema Ngonyo.

Aidha aliwataka wananchi kuacha dhana potofu ambazo zimeanza kusambaa katika mitandao ya kijamii na kwamba wameamua kuunga mkono juhudi za Serikali hivyo shughuli za hoteli zinatarajiwa kuanza tena mwishoni mwa Mei.

Mmoja wa wafanyakazi katika hoteli hiyo, Hadija Ramadhani, alisema kuwa wamelazimika kuunga mkono maagizo ya Serikali ili kupunguza maambukizi kwa wafanyakazi pamoja na wananchi ambao wanaweza kufika katika hoteli hiyo kupata huduma.

“Tunaomba watu waachane na habari za mitandao kwani zinatuchafua, lakini lengo letu ni kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wetu pamoja na wateja ambao wanakuja kupata huduma katika hoteli yetu,” alisema Hadija.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles