31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

NEC yawataka wananchi wajitokeze uhakiki daftari la wapigakura

Mwandishi Wetu -Dar es salaam

WANANCHI waliojiandikisha katika Daftari la Wapigakura mwaka 2015 na wale waliojiandikisha katika uboreshaji wa daftari hilo awamu ya kwanza, wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhakiki taarifa zao pindi litakapowekwa wazi katika maeneo yao na watumie njia nyingine za uhakiki kama ilivyoelekezwa.

Ushauri huo umetolewa jana Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage alipokuwa akifungua mkutano ulioandaliwa na tume na vyama vya siasa kuweka wazi mabadiliko yaliyojitojeza kwenye daftari la awamu ya pili la kupigia kura na kukabidhi nakala kwa wawakilishi wa vyama vya siasa.

Jaji Kaijage alisema uboreshaji huo utaanza Aprili 17 na kukamilika Mei 4, kwa nchi nzima ambapo wamegawa katika ruti tatu na kufanyika kwa siku tatu kwa kila mkoa kwa Tanzania Bara na Visiwani.

Alisema jumla ya vituo vitakavyotumika awamu hii ni 4,006 badala ya 8,031 vilivyokuwa vimekubaliwa awali ambapo kwa sasa vituo  3,956  vitakuwa Tanzania Bara na 50 Zanzibar.

Aidha alisema uboreshaji huo utafanyika katika kila kata ambapo kutakuwa na mwandishi msaidizi na BVR Kit Operator ambao watakuwa na orodha ya vituo vyote katika kata husika na watendaji hao watakuwa na uwezo wa kuboresha taarifa za mpigakura yeyote.

Alisema wananchi hususani wenye sifa ya kujiandikisha kama wapigakura wapya wasisubiri kujitokeza siku ya mwisho ya zoezi na hivyo kusababisha msongamano bali wafike vituoni mara tu zoezi litakapowafikia na watuze kadi zao.

Sambamba na hayo, Jaji Kaijage alisema NEC haina wataalamu wa afya ila imenunua vifaa vya kujikinga kwa kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa corona unaosababishwa na virusi vya Covid-19 na tayari wametoa maelekezo kwa watendaji wake kuzingatia miongozo ya wataalamu wa afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles