New Delhi, India
Nchi ya India leo Mai 24, 2021 imetangaza kuwa imevuka kizingiti vifo vya watu 300,000 kutokana na ugonjwa wa Corona, na kuwa nchi ya tatu duniani kufikia takwimu hii, baada ya Marekani na Brazil.
Katika wiki za hivi karibuni, India ilirekodi mara kwa mara idadi ya kila siku ya visa vya maambukizi na vifo huku idadi ya visa vya maambukizi imezidi milioni 26.7, idadi inayoshangaza, hata ikilinganishwa na idadi ya watu wote ambayo ni wakazi bilioni 1.3.
Ndani ya muda wa saa 24 zilizopita, nchi hiyo ilirekodi vifo vipya 4,454 kutokana na virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19, ikiwa ni ripoti ya pili ya kila siku ya idadi ya juu zaidi tangu rekodi ya vifo 4,529 kufikia siku ya Jumatano.
Maiti za watu wanaoshukiwa kuwa waathiriwa wa Corona zilipatikana zikielea kwenye maji ya Ganges au kuzikwa kwenye makaburi ya kina kirefu.