23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

Watu 15 walitopiwa kufariki Congo

Kinshasa, DRC

Nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeripotiwa takriban watu 15 wamethibitishwa kufariki kutokana mlipuko wa volkano uliotokea katika Mlima wa Nyiragongo, mashariki mwa nchi hiyo.

Mlipuko huo wa Volkano uliotokea siku ya Jumamosi Mai 22, 2021 huku ikidaiwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka wakati maafisa wakiyafikia maeneo yaliyoathirika zaidi.

Msemaji wa serikali Patrick Muyaya siku ya Jumapili Mai 23, 2021 alisema volkano hiyo ililipuka katika mlima Nyiragongo na kumwaga ujiuji wa moto ama lava uliolifanya anga kuwa na rangi nyekundu lakini lava hiyo haikufika katika mji wa Goma wenye watu milioni mbili kusini mwa mlima huo.

Pia wakazi wa vijiji vya karibu na mlima huo pamoja na mji Goma ambao waliyakimbia makazi yao kwa hofu ya mlipuko huo wameanza kurejea huku wengi wao wakiwasaka jamaa zao waliopotea.

Muyaya aliongezea na kusema watu tisa miongoni mwa waliothibitishwa kufa, walipoteza maisha katika ajali za barabarani, wakati watu wakikimbia ili kuokoa maisha yao.

Wanne walikufa walipokuwa wakijaribu kutoroka gerezani huku wawili wakiungua hadi kufa.

Zaidi ya watoto 170 wanahofiwa kupotea na wengine 150 wametengana na familia zao, kulinga na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef) ambalo linasema litaweka vituo vya kuwapokea watoto watakaopatikana wakiwa peke yao.

Lava iliishia karibu na wilaya ya Buhene, viungani mwa mji wa Goma na kuangamiza mamia ya nyumba na hata majengo makubwa. Ukarabati unatarajiwa kuchukua miezi kadhaa.

Pia lava ilikatiza katika moja ya barabara kuu inayounganisha Goma na mji wa Beni, ambayo ni njia muhimu ya usambazaji wa misaada.

Hata hivyo, uwanja wa ndege wa wa mji wa Goma haukuguswa na lava, kinyume na ripoti za awali kwamba uliathiriwa.

Mlima huo wa volkano uliopo kilomita 10 kutoka Goma, ulilipuka mara ya mwisho mwaka 2002 na kusababisha vifo vya watu 250 huku watu wengine 120,000 wakiachwa bila makazi.

Mlipuko wa volkano uliosababisha vifo zaidi ulitokea mwaka 1977, ambapo watu 600 waliuawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles