23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Wasafiri 90 kutafutwa Nigeria

Abuja, Nigeria

Serikali ya Nigeria imetangaza watu 90 wanatafutwa kwa kukiuka kanuni za karantini zilizowekwa kukabiliana na ugonjwa wa Covid 19 nchini humo.

Watu hao ambao wanigeria 63 na raia 27 wa kigeni waliongia nchini humo Mei kati ya tarehe 8 na 15, 2021 ambao wanaripotiwa kukataa kufanyiwa vipimo vya corona na uchunguzi zaidi.

Taarifa iliyotolewa na kamati iliyoteuliwa na rais kushughulikia ugonjwa wa covid 19, imesema watuhumiwa wanakabiliwa na vikwazo, vinavyojumusha kupigwa marufuku ya usafiri kwa mwaka mmoja na kufutiwa viza zao na vibali kwa raia wa kigeni na kushtakiwa.

Kamati hiyo iliongezea na kusema kuwa watu hao ni tisho kwa usalama wa afya ya umma kwani wamekwepa masharti ya karantini ya siku saba iliyowekwa kwa watu wanaowasili kutoka nchi zilizowekewa vikwazo vya usafiri na kuwaagiza wasafiri kujiwasilisha katika vituo vya afya vya umma ndani ya saa 48 ili kufanyiwa uchunguzi haraka iwezekanavo.

Mapema mwezo huu, Kamati hiyo ya ushauri wa rais ilitoa ilani ya usafiri kwa wasafiri wanaowasili nchini Nigeria kutoka Brazil, India na Uturuki.

Wasafiri kutoka nchi hizo tatu walitakiwa kuenda karantini ya lazima na kufanyiwa vipimo vya kubaini hawana maambukizi ya corona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,244FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles