26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Corona yaendelea kutafuna India

New Delhi, India

Nchi ya India leo Mai 24, 2021 imetangaza kuwa imevuka kizingiti  vifo vya watu 300,000 kutokana na ugonjwa wa Corona, na kuwa nchi ya tatu duniani kufikia takwimu hii, baada ya Marekani na Brazil.

Katika wiki za hivi karibuni, India ilirekodi mara kwa mara idadi ya kila siku ya visa vya maambukizi na vifo huku idadi ya visa vya maambukizi imezidi milioni 26.7, idadi inayoshangaza, hata ikilinganishwa na idadi ya watu wote ambayo ni wakazi bilioni 1.3.

Ndani ya muda wa saa 24 zilizopita, nchi hiyo ilirekodi vifo vipya 4,454 kutokana na virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19, ikiwa ni ripoti ya pili ya kila siku ya idadi ya juu zaidi tangu rekodi ya vifo 4,529 kufikia siku ya Jumatano.

Maiti za watu wanaoshukiwa kuwa waathiriwa wa Corona zilipatikana zikielea kwenye maji ya Ganges au kuzikwa kwenye makaburi ya kina kirefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles