19.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Conte ana matumaini ya kutua Chelsea

antonio-conte-1London, England

KOCHA wa timu ya taifa ya Italia, Antonio Conte, ana matumaini ya kuthibitishwa kuwa kocha wa muda mrefu wa timu ya Chelsea, kabla ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Hispania Machi 24, mwaka huu.

Kocha huyo anaamini anaweza kutua kwenye klabu hiyo na kupata mkataba wa miaka mitatu na kuwazidi makocha wengine waliokuwa wakihitajika na klabu hiyo.

Wawakilishi wake ambao walikuwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Chelsea bado wanaendelea na mazungumzo hayo, ambapo msingi wake ni kupatikana kwa kocha atakayechukua nafasi ya kocha wa mpito wa sasa, Guus Hiddink, mwishoni mwa msimu.

Mkataba wa kuifundisha timu ya taifa ya Italia unakwisha mwishoni mwa msimu huu baada ya michuano ya Ulaya hivyo kocha huyo huenda akapewa mkataba mpya kutoka Shirikisho la Soka la Italia (FA).

Italia watakutana na Hispania na baada ya siku tano watakutana na Ujerumani, ambapo Conte angependa hadi wakati huo dili lake liwe tayari limekamilika kabla ya michezo ya kirafiki ya kimataifa kuanza.

FA imekuwa katika mchakato wa kuandaa mkataba mpya wa kocha huyo ili kubaki na timu ya taifa hadi Kombe la Dunia mwaka 2018, lakini Conte (46) anaonekana kuwa na hamu ya kutaka kutua Chelsea.

Awali Chelsea ilikuwa na matarajio ya kuinasa saini ya kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeon, Jorge Sampaoli na Massimiliano Allegri, lakini imeonekana kuwa Conte ndiye chaguo lao la kwanza.

Kupatikana kwa kocha wa timu hiyo inaweza kuwa nafasi ya Juan Cuadrado, ambaye anatumikia usajili wake wa mkopo kwenye klabu ya Juventus.

Cuadrado anatarajia kupata usajili wa moja kwa moja na miamba hiyo ya Italia, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 bado anayo nafasi ya kumshawishi kocha mpya wa Chelsea.

Hata hivyo, kwenye tukio jingine Mkuu wa Ufundi wa Chelsea, MichaelĀ  Emenalo, alionekana kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliokuwa ukichezwa na Juventus dhidi ya Bayern Munich, ambapo walikutana na Conte huku kukiwa na taarifa ya usajili wa Paul Pogba na Arturo Vidal majira ya kiangazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles