22.5 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Zidane na Simeone wakumbushia fainali ya UEFA

Zinedine ZidaneMadrid, Hispania

UPANDE mmoja Zinedine Zidane, mwingine Diego Pablo Simeone, hakuna zaidi ya kuzitaka pointi tatu  muhimu kwenye  mchezo wa Ligi Kuu Hispania, La Liga.

Mchezo huo wa watani wa jadi wa jiji la Madrid utazikutanisha timu ambazo moja ipo nafasi ya pili, nyingine ya tatu, huku ukiwakumbusha mashabiki wa timu hizo fainali ya Ligi ya  Mabingwa Ulaya uliochezwa mwaka 2013/14.

Makocha hao wanakutana huku kila mmoja akicheza aina tofauti na mwingine ambapo waliwahi kufanya hivyo kabla ya kuwa makocha.

Zidane anaonekana mwenye kipaji zaidi ya Simeone, ambaye ameonekana kuwa mfano sahihi wa soka la Argentina.

Kwa sasa Zidane anatumia mfumo wa 4-3-3, huku akiwa na fikra za kumiliki mpira zaidi, lakini Simeone ameweza kutengeneza ushindani wa nguvu kwenye timu yake na kuzitisha timu kubwa kwenye ligi hiyo.

Licha ya utofauti mkubwa unaoonekana  katika ya timu hizo, kuna kitu kimoja ambacho makocha hao wanafanana.

Ni dhahiri kwamba, wachezaji wa Real wanapambana ili kulinda heshima ya timu yao, sawa na wachezaji wa Atletico, lakini leo itatosha kumaliza  ubishi dhidi ya wakongwe hao.

Zidane alijiunga  Real akiwa  na umri wa miaka 29 akiwa mchezaji na kusababisha kila shabiki wa timu hiyo kumpenda na zaidi watalikumbuka zaidi bao lake alilofunga kwenye fainali ya Kombe la Ulaya.

Simeone akiwa ‘Rojiblancos’ katika vipindi viwili tofauti, awali alikuwa mchezaji bora wakati Atletico ikichukua makombe mawili, likiwamo la Ligi Kuu, La Liga kwa mara ya kwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles