27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Hiddink kuendeleza rekodi leo?

guus-hiddink-getLONDON, ENGLAND

KOCHA wa timu ya Chelsea, Guus Hiddink, atakuwa mwenye kuhitaji kuweka rekodi kwenye timu hiyo kutokana na minong’ono juu ya kocha wa Italia, Antonio Conte, kuwa mbioni kujiunga  na klabu hiyo.

Chelsea itakuwa ugenini kucheza na Southampton kutafuta pointi tatu ili kupata nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kocha wa timu ya Southampton, Ronald Koeman, rekodi yake ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Chelsea itamfanya kuwa na matumaini ya kupata ushindi mwingine akiwa nyumbani.

Hata hivyo, Hiddink aliweza kuiongoza vema klabu hiyo na kuifanya kuwa kwenye kiwango kizuri tangu kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho.

Chelsea inaonekana kuwa imara kwa kufanikiwa kupata ushindi kwenye michezo 11 ya Ligi Kuu England bila  kufungwa na timu ya Southampton.

Chelsea ipo nafasi ya 12, ikiwa na tofauti ya pointi saba dhidi ya Southampton, iliyoko nafasi ya sita, ikiwa na pointi 40.

LEICESTER CITY VS NORWICH CITY

KOCHA wa timu ya Leicester City, Claudio Ranieri, tayari ameonesha ari ya kujiamini  na kuwataka wachezaji wake kuondoa presha kwenye  mchezo dhidi ya Norwich City ili kufanikiwa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Ranieri alishuhudia kikosi chake kikichapwa mabao 2-1 dhidi ya Arsenal wiki iliyopita, huku baadaye akirejesha  matumaini ya kufanya vizuri Ligi Kuu baada ya kuondolewa kwenye michuano ya kombe la FA.

Baada ya Norwich kutua kwenye Uwanja wa King Power, Leicester wanatarajia kukutana na West Brom, Watford, Newcastle United na Crystal Palace kabla ya michezo ya kimataifa kuchezwa.

Norwich walishinda mchezo mmoja tu tangu mwaka kuanza, mara ya mwisho walitoka sare 2-2 dhidi ya West Ham katika Uwanja wa Carrow.

Manchester United VS Arsenal

Mchezo ambao unatarajia kuwa wenye kuvuta hisia za mashabiki ambapo Arsenal itakuwa mgeni wa Manchester United katika Uwanja wa Old Trafford.

Hata hivyo, mchezo huo ambao utakuwa  mgumu kwa timu zote, Arsenal watahitaji pointi  tatu ili kuongeza mbio kuelekea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.

Tottenham VS Swansea

Spurs wapo nafasi ya pili, ikiwa na tofauti ya pointi mbili tu na vinara wa Ligi Kuu England, Leicester City, hivyo wanahitaji kuwapa presha wapinzani wao.

Pia timu ya Swansea wanaonekana  kuhitaji pointi zozote kutoka kwa Spurs ili kuondoka kwenye hatari ya kushuka daraja msimu huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles