Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Coca Cola imekabidhi soko la wafanyabiashara wadogo 100 ‘’wamachinga’ kwa Serikali walilojenga eneo la Kigogo Dampo, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kufungua soko hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ameipongeza kampuni hiyo kwa kuunga mkono Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
“Mmejuwa kutufariji wakati wa shida, tukiwa tupo kwenye changamoto ya machinga ndio mmeweza kutufikiria na kutukabidhi soko, sisi kama serikali tutahakikisha tunalitanua na kuwa kubwa zaidi ili kuchukua wafanyabiashara wengi.
” Tutahakikisha hata magari yanakuja na kuleta watu waweze kununua vitu kwa wafanyabiashara watakaokuwa humu,” amesema Makalla.
Aidha amewashukuru kwa kuwa wamekuwa ni watu wanao wakimbilia na kuwasaidia katika kila changamoto, kwani waliweza kujenga vibanda Coco beach na sasa wamejenga soko Kigogo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Kwanza, Unguu Sulay, amesema kuwa waliona ni vizuri kuweza kujenga soko ili kurahisisha wakazi wa Kigogo na maeneo ya karibu kupata mahitaji.