MWANAMUZIKI wa miondoko ya Pop na RnB nchini Marekani, Christina Aguilera, amesema ana vigezo vitatu vinavyomfanya avutiwe na msanii mwezake, Janet Jackson.
Akizungumza na Jarida moja maarufu la burudani nchini humo, Christina alisema alipokuwa mdogo alikuwa akimfuatilia Janet Jackson kwenye runinga na alijikuta akivutiwa naye hadi alipoingia katika muziki akaendelea kuvutiwa naye.
“Nilikuwa napenda anavyocheza kwenye video zake na zaidi ilikuwa sauti yake ya kimahaba ‘Sexiest Voice’ ndiyo ilikuwa inanikosha mno,” alisema Christina na kuongeza kuwa ndiyo maana anajituma ili amfi kie mafanikio yake
kimuziki.