30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Kampeni za Fella burudani zatawala

felaWAKALI wa muziki wa Bongo Fleva, juzi walifunga kampeni za mgombea udiwani wa Kata ya Kilungule, Mbagala, jijini Dar es Salaam, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Said Fella kwa kupagawisha wakazi wa eneo hilo kwa onyesho la aina yake.

Shamra shamra za wakazi wa eneo hilo zilianza baada ya kusikika uwepo wa wasanii maarufu na wenye majina
makubwa nchini akiwemo, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, Nurdin Bilal ‘Shetah’, Hamis Mwinjuma ‘Fa’, kundi la Yamoto na wengine wengi.

Baadhi ya wasanii hao walipomaliza kutumbuiza waliwaomba wananchi hao wamchague Fella kwa madai kwamba ataweza kuwafikisha mbali kimaendeleo kama alivyoweza kumsaidia msanii Diamond kufikia malengo yake katika muziki anaofanya.

Naye Fella aliwataka wananchi hao wampigie kura za kutosha ili aweze kushirikiana nao kusaka maendeleo kuwa anafahamu changamoto zote zinazowakabili wakazi wa eneo hilo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,391FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles