MWANAMUZIKI Taylor Swift ametajwa kugombea katika vipengele sita vya tuzo za muziki za American Music Awards (AMAs) za huko Marekani.
Taylor amewapiku The Weekend na Ed Sheeran, waliotajwa katika vipengele vitano, Nicki Minaj, Sam Smith
na Meghan Trainor, wametajwa mara nne ambapo Drake, Chris Brown na Fetty Wap wametajwa mara mbili.
Sherehe za utolewaji tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika Novemba 22 mwaka huu nchini Marekani.