Christian Bella leo kunogesha Shinyanga Day

0
753

christian bellaNA THERESIA GASPER

MSANII wa Bolingo, Christian Bella, anatarajia kutumbuiza katika siku ya Shinyanga Day, inayotarajiwa kufanyika kesho Mjini Shinyanga.

Akizungumza na MTANZANIA, Ofisa Habari wa Klabu ya Stand United, alisema wameona wamuite msanii huyo ili aje kutoa burudani kwa mashabiki wake katika sherehe hizo ili waweze kupata burudani zaidi.

“Pamoja na Christian Bella kuja kutupa burudani kutakuwa na mambo mbalimbali ya kuwafurahisha mashabiki wetu, hivyo tunawaomba wajitokeze kwa wingi,” alisema.

Msanii huyo amefanikiwa kufanya vizuri katika wimbo wake wa Nani kama Mama, alioshirikiana na msanii mwenzake, Omary Faraji ‘Ommy Dimpoz’ ambao umeonekeana kuwagusa mashabiki wake wengi, hususan kina mama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here