22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Tamasha jipya la burudani la KiliFest kuzinduliwa Dar

rubyNA FESTO POLEA

TAMASHA jipya la burudani la KiliFest linatarajiwa kuzinduliwa Septemba 26, katika viwanja vya Leaders Club, ambapo idadi kubwa ya wasanii wa Bongo Fleva nchini watatumbuiza.

Tamasha hilo linakuwa la kwanza kwa Tanzania na litaanzia jijini Dar es Salaam, lakini kwa miaka ijayo litazunguka na mikoa mingine.

Meneja  wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli, ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo, alisema lengo la tamasha hilo ni kuwaleta Watanzania pamoja kupitia burudani na michezo mbalimbali itakayopatikana katika tamasha hilo.

Pia Kikuli aliwataja wasanii watakaoshiriki katika tamasha hilo kuwa ni Mapacha Watatu, Maua, Ruby, Damian Soul, Vanessa Mdee, Ben Pol, Weusi, Fid Q, Isha Mashauzi na Shettah.

Licha ya muziki, Kikuli alisema pia kutakuwa na vyakula na vinywaji mbalimbali pamoja na matukio ya kufurahisha na kuburudisha, ikiwemo michezo ambayo washindi wake watapata fursa ya kuwa karibu na kuzungumza na wasanii watakaotumbuiza siku hiyo.

“Kilifest ni tamasha la aina yake na halijawahi kutokea Tanzania, ni matumaini yetu kuwa Watanzania watajitokeza  kwa wingi katika viwanja vya Leaders kwa kiingilio cha Sh 10,000,” alisema Kikuli.

Naye msanii Ruby kwa niaba ya wasanii wenzake alisema siku hiyo wasanii wote watatumbuiza kwa kutumia bendi, hivyo muziki wao utakuwa wa ‘live’ na si kutumia CD ‘Play back’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles