30.2 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Christian Bella kunogesha usiku wa Valentine

christian bellaNA OSCAR ASSENGA, TANGA

MSANII wa muziki wa dansi nchini, Christian Bella, anatarajiwa kutumbuiza kwenye onyesho maalumu la usiku wa mkesha wa Sikukuu ya Wapendanao, uliopewa jina la Red & White Party Valentine Day kwenye ukumbi wa Harbours.
Mratibu wa Onyesho hilo, Mbwana Imamu, alisema onyesho hilo litaanza saa mbili usiku wa Februari 13 hadi siku ya wapendanao Februari 14, ambapo wapenzi na mashabiki wa muziki watapata burudani ya nyimbo mahiri za Christian Bella, ukiwemo wimbo wa ‘Nagharamia’ na ‘Amerudi’.

“Unajua hilo onyesho litakuwa maalumu kwa usiku wa mkesha wa Sikukuu ya Wapendanao kwa sababu lazima wapate burudani nzito za kusindikiza siku hiyo maalumu ambayo ni muhimu kwa wapendanao, lakini
pia watapata nafasi ya kukaa na kufurahia mambo yatakayokuwa yakifanyika,” alisema Imamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles