27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

20 Percent: Muziki wangu si wa kushindana

20PNA GLORY MLAY

MKALI wa muziki wa Bongo Fleva aliyewahi kunyakua tuzo 5 za Kili, Abas Kinzasa ‘20 Percent’, anatarajiwa kuibuka upya na wimbo wa ‘Mbaya hana Sababu’.

Wimbo huo kwa sasa anaendelea kukamilisha video yake anayoamini itakamilika kabla ya mwishoni mwa mwezi huu.

Hata hivyo, licha ya ukimya wake, 20 Percent anadai kwamba muziki wake si wa kushindana na msanii mwingine yeyote, ndiyo maana mwenendo wake katika muziki huo ni wa taratibu.

“Mimi sishindani na mtu katika muziki wangu, nafanya muziki wangu ninavyojisikia, moyo ukitaka naingia studio natoa, lakini nyimbo zangu zote nina hakika zitazoa mashabiki kwa kuwa ujumbe wangu ni wa kueleweka na upo tofauti na wasanii wengine,’’ alijinadi.

Msanii huyo aliongeza kwamba, wimbo wake mwingine wa ‘Mapenzi Sina’ alioukamilisha ‘audio’ yake pia anataraji kuufanyia video yake hivi karibuni.

“Mimi sijapotea, ninarudi na nyimbo hizo na nimeshatoa huo wimbo wa ‘Mapenzi Sina’ ambao nao nakamilisha video yake, lakini kwa sasa sina studio maalumu, narekodi studio yoyote inayoweza kufanya muziki wa aina yangu,’’ alieleza 20 Percent.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles