NEW YORK, MAREKANI
MWIGIZAJI maarufu nchini Marekani, Chris Rock, ameachana na mke wake, Malaak, baada ya kukaa miaka 20 katika ndoa yao.
Rock, ambaye amekuwa mshereheshaji katika matamasha mbalimbali ya Black Entertainment Television (BET), inadaiwa kwamba alianza kugombana na mke wake tangu mwaka 2014, lakini mwanzoni mwa wiki hii wameweka wazi kuachana kwao.
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 51, alifanikiwa kupata watoto wawili wa kike akiwa na mrembo huyo, ambao ni Lola Simone mwenye umri wa miaka 14 pamoja na Zahra Savanna, mwenye umri wa miaka 12.
Mtandao wa TMZ umedai kwamba wawili hao tayari wameachana tangu Jumatatu, lakini hadi sasa hawajataka kuweka wazi, ila watu wa karibu na familia hiyo wamesema tayari wameachana.