MKALI wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, amesema mtoto wake, Royalty, amembadilisha kitabia na mfumo wake wa maisha kwa sasa.
Awali msanii huyo alikuwa akitumia muda mwingi kufanya mambo yasiyo na maana kwa jamii na familia yake, lakini tangu alipoanza kumlea mtoto huyo amekuwa na mabadiliko makubwa katika maisha yake.
“Royalty amekuwa na mchango mkubwa wa kubadilisha maisha yangu, kutokana na hali hiyo ninatakiwa kumfanyia kila kitu ambacho anapaswa kufanyiwa.
“Maisha yangu ya sasa yamekuwa ya kiutu uzima ila haya yote yanatokana na kuitwa baba,” alieleza Chris.
Msanii huyo kwa sasa anatamba na wimbo wa ‘Zero’, wiki iliyopita aliachia albamu yake mpya ‘Mix tap’ yenye wimbo alioshirikiana na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Rihanna.