27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Kobe Bryant atangaza kustaafu kikapu

BKN-NBA-GRIZZLIES-LAKERSNEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa kikapu wa timu ya Los Angeles Lakers, ambayo inashiriki Ligi Kuu NBA ya nchini Marekani, Kobe Bryant, ametangaza kustaafu mchezo huo mwishoni mwa msimu huu.

Bryant, mwenye umri wa miaka 37, amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu yake kwa kuipa ubingwa wa Ligi hiyo, lakini kutokana na umri wake kuwa mkubwa amedai huu ni msimu wake wa mwisho.

Nyota huyo amewahi kuchukua tuzo mbalimbali, ikiwa pamoja na ile ya Olympic Gold Medals mara mbili, wakati huo akichukua tuzo ya championship rings mara tano, huku akiitwa katika kikosi cha wachezaji bora wa NBA mara 17. 

Msimu uliopita alisema msimu huu wa 2015/16 atahakikisha anaipa timu yake yale yote ambayo inatakiwa kupata katika michuano hiyo.

Hata hivyo, anaamini kuwa kuondoka kwake kutawapa nafasi wachezaji wengine kuendelea kufanya vizuri kutokana na kile ambacho amekifanya kwa miaka yote.

“Moyo wangu hauwezi kuendelea kuwa kwenye kikapu, akili yangu haiwezi kudumu kwenye mchezo huu, lakini mwili wangu kwa sasa unajua kwamba huu ni muda wa kusema kwa heri.

“Huu ni muda wangu wa kuondoka, nataka kila mmoja ajue hivyo, lakini tutaendelea kuwa pamoja katika mambo mengine mbalimbali.

“Ninaamini kuondoka kwangu kutawapa nafasi wachezaji wengine kufanya vizuri kwa kuwa ninaamini wapo ambao wanafanya vizuri kwa sasa, hivyo huo ni wakati wao,” aliandika Bryant.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles