28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Chiku Abwao avinjari viwanja vya Bunge

Mbunge wa Chadema, Chiku Abwao
Mbunge wa Chadema, Chiku Abwao

NA MWANDISHI WETU, DODOMA

WAJUMBE wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wameendelea kumiminika mjini hapa, unakoendelea mkutano wa Bunge Maalum la Katiba, ambao umoja huo umesusia.

Jana Mbunge wa Viti Maalum, Chiku Abwao (Chadema), alionekana ndani ya viwanja vya Bunge.

Hata hivyo, mbunge huyo alisema alifika kwenye viwanja hivyo kwa lengo la kuchukua gari lake alilokuwa ameliacha na si kuudhuria mkutano wa Bunge la Katiba unaoendelea.

Alisema amekuwa mwanamapinduzi kwa muda mrefu na kuwa hawezi kurejea kwenye Bunge linaloendelea kwa kuwa yeye ni mwana Ukawa damu.

Lakini jana ilidaiwa kuwa baadhi ya wajumbe wa CUF kutoka Zanzibar walikuwa mjini hapa, ingawa hawajafika bungeni kujiandikisha na kuendelea na mkutano huo.

Baadhi ya wajumbe wanaohudhuria mkutano huo, wanaamini kuwa wajumbe wa Ukawa watarudi kuendelea na mkutano huo, na ndiyo maana baadhi yao wapo mjini hapa kusubiri viongozi wao walegeze msimamo.

“Watakuja tu hawa, si umeona ratiba kupiga kura kuko mwisho kabisa, lazima tu wanabanwa na njaa warudi, wengi tu wapo Dodoma wanasikilizia wakubwa wao walegeze kamba,” alisema mmoja wa wajumbe wa Bunge hilo.

Akizungumza juzi usiku baada ya kikao cha Kamati ya Uongozi, Katibu wa Bunge hilo, Yahaya Hamasi, alisema watafanya kazi ya kupitia majina ya wajumbe waliojiandikisha ili kuona kama kati yao wapo wa Ukawa.

Alisema amesikia kuwa kuna baadhi ya wajumbe wa Ukawa ambao wamejiandikisha, lakini hana uhakika na hilo.

Hadi kufikia juzi saa 10 jioni, wajumbe 226 ndio waliokuwa wamejiandikisha kati ya 628 waliopo.

Alisema ili Bunge hilo lianze kufanya kazi, inatakiwa wajumbe 314 wawe wamefika.

“Kesho tutaangalia kama tutakuwa tumefika idadi ya kutosha tutapitia kanuni hizo,” alisema.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, akizungumza jana wakati wa kufungua Bunge, alisema kuwa wajumbe waliowasili ni zaidi ya robo tatu ya wajumbe wote wa Bunge hilo.

- Advertisement -

Related Articles

2 COMMENTS

  1. Duh! Rangi zote za Sitta kama kiongozi zimedhihirishwa na uenyekiti wake wa bunge la katiba. Mbio zake kuwa raisi wetu zimegota hapa. Apumzike kwa amani.

  2. Ukawa tunaomba mrudi bungeni, ili mpate nafasi ya kutoa maoni yenu, na mpate nafasi ya kuzidi kutetea katiba yetu, mkiwa nje mtashindwa kutuwakilisha na hoja zetu mtazisemea wapi? Rudisheni roho zenu nyuma, kwa kawaida huwa kuna mmoja lazima ajishushe kwa mwingine ili kukwepa ugomvi na kufikia muafaka. Tunajua mlio nayo mkiyasema yatasikilizwa, kwa sababu kila mtanzania ameshajua kwa nini mko nje ya bunge la katiba. Hivyo bunge la katiba halitakuwa na upinzani kama mwanzo, kwani sisi watanzania hatukuwa tunajua mnashindwa kuelewana nini, lakini kutokana na mikutano ya hadhara angalau tumeweza kupata picha ya nini kinazungumzwa. UKWELI TUNAUMIA KUONA PESA ZA POSHO ZILISHAANZA KUTUMIKA KUWALIPA WABUNGE WOTE WA BUNGE LA KATIBA, INAFIKA MAHALI ETI WENGINE WAPO NJE, INA MAANA PESA ILE IMEPOTEA BURE, HAMNA KILICHOJADILIWA CHA MAANA. TUNAUMIA KODI ZETU JAMANI.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles