23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mtoto wa ajabu azaliwa Dar

Hospitali ya Mwananyamala
Hospitali ya Mwananyamala

NA VERONICA ROMWALD, DAR ES SALAAM

MTOTO wa ajabu anayedaiwa kuzaliwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam ameibua mjadala mkubwa katika jamii.

Taarifa zilizoenea jana katika mitandao ya kijamii zilionyesha picha ya sura ya mtoto huyo akiwa na umbo la binadamu, lakini macho yake na sura akiwa anafanana na chura.

MTANZANIA ilifika katika Hospitali ya Mwananyamala na kukuta taarifa zikiwa zimezagaa kuhusu tukio hilo linalovuta hisia za watu.

Inadaiwa mtoto huyo mwenye jinsia ya kiume alizaliwa katika hospitali hiyo usiku wa Agosti 4, mwaka huu, na kwamba madaktari walipomuona walipigwa butwaa kwa kushangaa maumbile yake.

Hadi tunakwenda mitamboni, viongozi wa hospitali hiyo hawakupatikana na kila wakati ilikuwa inaelezwa kuwa walikuwa kwenye kikao.

Hata hivyo, mmoja wa viongozi wa Bodi ya Afya ya hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini kwa kuwa si msemaji, alisema taarifa za kuzaliwa kwa mtoto huyo zimewashtua na kulazimika kuunda tume kulishughulikia suala hilo.

“Mimi mwenyewe nimeona picha hiyo iliyotumwa mtandaoni ikisema mtoto huyo alizaliwa hapa hospitalini, na nyingine ikieleza kwamba amezaliwa katika Hospitali ya Temeke. Mimi nasema hivi, hapa Mwananyamala hakuna tukio hilo.

“Lakini kutokana na kusambazwa picha hiyo mtandaoni, tumefanya kikao cha ndani na tumeunda tume kuweza kubaini ukweli wa jambo hili na hata watu walioweka hii picha mtandaoni,” alisema.

Alisema kwa kawaida madaktari wanaweza kupiga picha ya mtoto wa aina hiyo chini ya umri wa miaka 18 kwa ruhusa ya mzazi wake, na iwapo amevuka umri huo analazimika kusaini ili apigwe picha na wao huitumia kwa ajili ya mafunzo na si kuiweka mtandaoni.

“Hata kama itatokea tukio kama hili, ni lazima madaktari wapate ruhusa ya mzazi mwenyewe na mara nyingi hutumika kwenye mafunzo. Lakini kama mhusika ametimiza umri wa miaka 18, huwa tunasaini naye makubaliano kwa mujibu wa sheria na miiko ya kazi yetu,” alisema.

Alisema kitendo kilichofanywa na mtu huyo aliyepiga picha na kuiweka mtandaoni, kinakiuka maadili na miiko ya kazi ya udaktari na ni cha udhalilishaji.

“Leo kwa sababu umeniuliza naomba ufahamu hivyo, kwamba tukio hili si la kweli na tumeunda hicho kikosi kazi kwa ajili ya kufanya uchunguzi, na kesho tutaeleza zaidi juu ya taarifa hii,” alisema.

Mmoja wa madaktari wa Hospitali ya Mwananyamala ambaye naye hakupenda jina lake litajwe gazetini, alisema matatizo kama hayo hutokana na hitilafu kwenye mfumo unaoanzia kichwani hadi kwenye uti wa mgongo.

Kwa mujibu wa daktari huyo, hitilafu hiyo husababisha mifumo ya mwili kuwa na dosari na hivyo kupatwa na hali kama hiyo.

“Katika nchi zilizoendelea madaktari bingwa na wenye vifaa vya kisasa wanaweza kuokoa maisha ya mtoto wa aina hii.

“Lakini hata kama mtoto huyo anaokolewa, atakabiliwa na tatizo kubwa la ulemavu wa akili kwa kuwa ubongo alionao ni nusu tu ya ubongo unaotakiwa kwa binadamu kamili,” alisema.

Alisema mjamzito anaweza kujifungua mtoto mwenye maumbile ya ajabu iwapo atakosa madini ya folic acid ambayo ni muhimu katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito wake.

“Mama anaweza kujifungua mtoto mwenye maumbile ya ajabu iwapo katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito wake atatumia dawa ya flagile, dawa za minyoo, ‘tetesakline’ na baadhi ya dawa za malaria kama vile SP ambayo anaruhisiwa kunywa baada ya wiki 28 na ALU ambayo hairuhusiwi kabisa kwa mjamzito.

“Kwa ujumla ni marufuku mama mjamzito kunywa dawa bila kumuona daktari,’’ alisisitiza daktari huyo.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Dk. Amani Malima, alipotafutwa alikanusha kutokea tukio la aina hiyo hospitalini hapo.

“Nimesikia taarifa ya kusambaa picha hiyo, lakini tukio hilo halijatokea hapa kwetu kama unavyoniambia,” alisema Dk. Malima.

- Advertisement -

Related Articles

3 COMMENTS

 1. shida ni kwamba habari za siku hizi huwez jua znatoka wap,, kama wahusika madaktar wamekanusha kuwepo kwa tukio hilo ni vp tuseme limetokea mwananyamala kama hatuna habari kamili

 2. asalaam alykum!, mimi leo nimeona nijitokeze kwa ajili ya kutoa maoni yangu kuhusiana na hili suala la KATIBA ninawashauri wajumbe wote waliopewa jukumu hili la utungaji wa katiba mpya wayazingatie yafuatayo:

  Wajue kuwa wao sio wananchi bora kuliko wenzao
  hii nchi sio yakwao peke yao
  kila mtu anayo haki sawa katika nchi yetu hii hivyo ni lazima kuangalia maslahi ya Taifa kuliko kitu kingine.

  hebu tuangaliae katika uhalisia mimi naona wajumbe wa bunge hili ambao ni kutoka CCM ambao ni wawakilishi kutoka znz wengi wao sio wakweli/ au labda kwa namna nyingine wanafuata pesa tu sio kitu kingine, kwanini nasema hivy: hebu chukulia katika hali ya akili ya kawaida tu zanzibar ilibadili katiba yao kwa minajili ya kutaka kupata mamlaka kamili, mimi labda sielewi unaposema mmlaka kamili maana yake nini?

  mamlaka kamili ni kutaka uhuru kamili wa kujiamulia mambo, hiyo ni lugha tu sasa ngoja tuangalie kama wawakilishi wote wanataka kupata mamlaka kamili leo iweje wawekwenye serikali mbili? mbona haiwezekani? maaana lazima serikali ya znz itakuwa inawajibika kwa serikali ya muungano ambayo kiukweli ndio Tanganyika, mimi naona hapa ni kiini macho, ndio wajumbe hao hao asubuhi CCM jioni UKAWA.

  Kwanini wanawayumbisha wananchi wao?

  POSHO ukiliangalia suala hili utaona kuwa hizo pesa wanazokwenda kuzitumia zinapotea bure kwani ni ukweli usiopingika kwamba KATIBA bila makubaliano haiwezekani hivi huyu mwenyekiti halioni hili? wakina Mwigulu/Saada na Malima pesa za wananchi mnazitumiaje? au kwasababu na nyinyi mpo humo kama sehemu ya kuzitafuna? jitahidini muwasiliane na Ras ili kulinusuru Taifa katika upotevu/ matumizi haya mabaya ya fedha za wananchi, ambazo zingeweza kuwasaidia katika mambo ya maendeleo yao. Siamini kama kweli hili bunge linaendelea ni maoni yangu hawa CCM wataona umuhimu wa kuachana na bunge hilo hadi maridhianao yatakapopatikana.

  Lingine wabunge wa bunge la Katiba jamani nyie sio Tanzania pekeyenu waacheni na wengine walizungumzie suala hili hiyo mamlaka mnapata wapi ya kutaka kuwaziba wenzenu midomo ili muendelee kuzitafuna pesa zetu, kila kukicha kodri siku zinavyoendelea halafu watu wazibwe mdomo kuwacha kujadili Kila siku kodi inaongezeka gemetrically wakiti kipato kinaongezeka arthmetically sio sawa hata kidogo. anayewaunga mkono nyiwe mlioko dodoma labda wale ambao hawailewi rasimu hii.

 3. NDUGU MHARIRI,

  naomba japo uniweke pembeni ya gazeti lako ili niweze kutoa yangu yalioko moyoni mwangu kwamba kiukwli yananiumiza sana

  kwanza kabisa mimi ninaona ili inchi hii iweze kusonga mbele inatakiwa kubadilika kimfumo kabisaa!! wala tusidanganyane kuwa sijui akiwa nani tutapata hiki mara kile hizo ni hadithi za alinacha,

  mfumo wa kitanzania ni mfumo wa uongozi wa kulindana hivyo kila mtu anajua fulani akiingia madarakani atanilinda ndio maana hata serikali haifanyi juhudi za dhati kabisa kuhakikisha kuwa elimu kwa wananchi wa kitanzania inazingatiwa kwa kiwango ambacho kinaweza kuwafanya waweze kujitambua na kujenga hoja.

  inaumiza sana maana katika kipindi hata cha kampeni za kisiasa utakuta vijana wengi ambao ndio Taifa linawategemea wanapatiwa kitu kidogo/pombe/chakula na kushindwa kabisa kijielewa kama kweli huyu mtu ananiaya dhati kunisaidia kwanini anishawishi nimpigie kura kwa kunipa vitu?
  sasa basi katika wakati huo wale jamaa ambao wanataka baadae walindwe ndio utakuta wanatoa pesa za kwenda kusaidia kampeni hizo chafu. mimi sio muongeaji sana wa mambo ya kisiasa lakini huwa nafuatilia sana habari zinazolihusu Taifa langu, utakuta mtu msomi mzuri leo anatoa hoja hii kesho anabadilika kabisa unamshangaa mfano kuna msomi mmoja simtaji aliwahi kuwaambia watu fulani kuwa mnakandamizwa hivyo mnahitaji kujitambua halafu huyo huyo akaonekana kuyakana maneno yake hii ni hatari kweli, lakini ukiaangalia wanaokuja kuumia ni vijana kwani hao viongozi tayari walijiwekea mambo yao vizuri na wanaimani kuwa hata wakiwepo nje ya ungozi watakuwa na watu wao watakaowalinda kutokana na mfumo uliopo. sasa vijana ndio waadhirika maana ndio kwanza na wao wanataka kujenga na wao mtandao ili wakizeeka nawao walindwe lakini kutokana na mfumo basi wanabaki kuteseka. Kuna viongozi nilikuwa nawasikia tangu sijajua mabaya na mazuri hivi hao kweli wanapaswa kuendelea kuongoza au kutoa ushauri halafu utakuta wao ndio wabishi kama nini kwenye kutoa maamuzi, hii nadhani wanafikiria kuwa wao mungu amewazaa kuwa Tanzania ni mali yao peke yao.

  MAONI YANGU

  Ninawashauri vijana wenzangu tusikubali kuburuzwa na kuwa makampeni manager ama wapambe wa wagombea ambao mwisho wa siku wanatuacha solemba na kutukabidhi kwa polisi na mgambo kutufukuza barabarani tusifanye biashara na kutupa jina la kejeli machinga hii sio sawa wao ndio walikuwa na jukumu la kuhakikisha kuweka mazingira mazuri ya kuhakikisha kuwa vijana wanafanya kazi zao bila kubugudhiwa na mtu yeyote, lakini wakatudharau.

  natoa wito kwa vijana kuwa katika mfumo huu tulionao wasitegemee mabadiliko yeyote kwa kiongozi yeyote atakayechaguliwa ilihali anatokea CCM, hawezi kubadili kitu chochote maana ni lazima awalinde wenzake walimfikisha hapo inafikia kulindana mpaka waziri na katibu mkuu hawaheshimiani tena.

  ni ngumu sana kwa kiongozi yeyote kutoka katika chama Tawala kuweza kuleta mabadiliko maana wenzake waliomzoea watamkwamisha tu! kwani watakuwa wanamuelewa vizuri, jamani tubadilike kwani vyama vyote vya siasa si watanzania wote wanazamira ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania? tuwachague wapinzani kwani mbona mambo mengi waliyoyaanzisha yamefanikiwa, mfano hoja ya kuhitaji katiba mpya niyawapinzani, wizi wa mabilioni nayo ni issue ya wapinzani. mimi kwa maoni yangu hawa wapinzani nao mpaka waje watengeneze mtandao wao tayari tutakuwa tumefika mahali kidogo katika maendeleo, maendeleo ya nchi hii ni ndoto tuking’ang’ania CCM hakuna wakuleta mabadiliko binadamu ameumbwa na haya atasema unajua huyu ni mwenzetu kubebana kama kawa viini macho lukuki, tuwape vijana lazima wataanza kuwawajibisha hao wote waliofanya makosa na italeta uwajibikaji kwa wananchi wetu na vijana watakuwa na utamaduni wa kujituma, sio sasa hivi mtu anataka kufanya kazi TRA, BANDARINI ili awe tajiri harakaharaka siku hizi rushwa sio siri kabisa unakwenda sehemu unaambia hapa hatujanywa chai lakini kwasababu unashida inabidi uache kitu kidogo. ninaimani watanzania ni waoga sana akiiingia mtu tofauti madarakani kila mtu atashika adabu, maana hawatafanya uzembe ule uliokidhiri kama sasa hivi.

  kwa sasa mtu akiharibu anajua mahali pa kukimbilia utasikia ngoja nikamwambie fulani ataongea na fulani basi limradi mambo yanakwenda shaghalabangala bora liende.

  hebu tubadilishe mbona wenzetu wamebadili na mambo yanakwenda hebu on UHURU kenyaja amekuwa wa kwanza katika uwajibikaji east africa yaani katika utendaji kazi mara baada ya kuondoa chama cha mzee mwai kibaki kila mtu aliyekuwa kwenye nafasi kama hana sifa ya utendaji tumbo joto.

  bila kuubadili huu mfumo tusitegemee kabisaaa kuyafaidi matunda ya Taifa letu hili huru wataendelea kufaidi walewale tuliokuwa tunawasikia tangu tukiwa wachanga kinachobadilika anatoka senior anakuja jounior, vijana na wananchi wote umaskini wa Tanzania tunajitakia bila kufanya Political change hakuna kinachoweza kubadilika/ tusidanganyike eti rais anasema yeye ndiyewa mwisho kuingoza Tanzania Maskini kwa ajili ya mapato ya gesi, hili nalipinga waziwazi pasipokuwa na viongozi wawajibikaji wanao muogopa mungu na waliotoka nje ya mfumo huu wa sasa wa CCM hakuna kitakachondelea itakuwa malalamiko mtindo mmoja, kwani Mnazi bay gas imebadilisha nini mimi kwa bahati nzuri nimetembelea sana maeneo haya ya kusini hakuna kilichobadilika, vijana tuachane na ushabiki wa kisiasa tuwe tunamaanisha kweli tunataka mabadiliko ya kweli lakini kwa maoni yangu bila kubadili huu mfumo hakuna kitu kitakachobadilika.

  haya ni maoni yang

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles