29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mzozo waibuka familia ya Mandela

Mke wa zamani wa Nelson Mandela, Winnie Mandela
Mke wa zamani wa Nelson Mandela, Winnie Mandela

Mwandishi Wetu na Mashirika ya habari

MTALIKI wa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Winnie Mandela ameibuka na kutaka watoto wake wapewe nyumba yake iliyoko kijijini Qunu.

Hatua yake hiyo huenda ikazua mgogoro wa kwanza wa kisheria kuhusiana na mali za Nelson Mandela tangu alipoaga dunia mwaka jana.

Mawakili wa Winnie Madikizela-Mandela wamesema kudai nyumba hiyo ni haki yake ya kiutamaduni kwa vile aliwahi kuwa mke wa marehemu Mandela.

Mali ya marehemu Mandela ilikadiriwa kuwa yenye thamani ya dola milioni 4.3 baada ya kifo chake Desemba mwaka jana.

Mzee Mandela alimpa talaka Madikizela-Mandela mwaka 1996 wakiwa wamefanikiwa kupata watoto wawili, Zinzi na Zenani.

Marehemu Mandela ana mtoto mwingine, aitwaye Makaziwe kutokana na ndoa yake ya kwanza kwa marehemu Evelyn Mase.

Wakati wa kifo chake alikuwa amemuoa, Graca Machel, mjane wa marehemu Samora Machel, aliyekuwa Rais wa kwanza wa Msumbiji.

Katika wosia wake, marehemu Mandela alisema: ”Mali yake ya Qunu ikiwemo nyumba hiyo inapaswa kutumiwa na familia yake nzima ili kukuza umoja katika familia hiyo ”

Lakini katika barua yake, Madikizela-Mandela anadai yeye ndiye aliyeipata nyumba hiyo katika eneo la Qunu, wakati Mandela alipokuwa gerezani akipigana baada ya kufungwa na uliokuwa utawala wa wazungu wachache.

“Msimamo wetu ni kwamba nyumba hiyo ni mali ya kizazi cha Mandela na Winnie Madikizela-Mandela,” ilisema barua hiyo.

“Ni katika nyumba hii pekee ambapo watoto na wajukuu wa Madikizela-Mandela wanaweza kuendesha shughuli zao, na nyumba hiyo haiwezi kukabidhiwa kwa mtu yeyote ambaye si mtoto wala mjukuu wake. ”

Barua hiyo ilisema kuwa haimaanishi kwamba watoto wengine wa Mandela watanyimwa ruhusa ya kuingia katika nyumba hiyo.

“Lakini udhibiti na usimamizi wa nyumba unapaswa kufafanuliwa kwa misingi ya kitamaduni na kimila,” walisema mawakili hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles