33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Chenge akata rufaa Mahakama Kuu

CHENGEPatricia Kimelemeta na Aziza Masoud
BARAZA la Maadili la Utumishi wa Umma jana lilikwama kuendelea na mahojiano na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM).
Baraza hilo lilishindwa kuendelea na kazi yake hiyo baada ya Chenge kukata rufaa Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga uamuzi wa Baraza hilo kuendelea kujadili tuhuma zinazomkabili.
bilioni 1.6 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Tanzania Ltd, James Rugemalira, kupitia Akaunti ya Tegeta Escrow.
Kabla ya shauri hilo kuanza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya
Utumishi wa Umma, Jaji mstaafu, Hamis Msumi, alisema baraza hilo lilipitia kwa makini zuio lililowasilishwa na Chenge juzi ili kujiridhisha kama ni kweli halina mamlaka ya kujadili suala lake.
Alisema kwamba baada ya kutafakari vifungu vya sheria, baraza hilo liliona zuio lililowekwa na Mahakama halihusiani na shughuli za baraza hilo bali linalikataza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na taasisi nyingine nane kujadili suala la miamala ya Escrow na wamiliki wake.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Msumi alisema baraza hilo liliamua kuendelea kumhoji Chenge liweze kujiridhisha na tuhuma zinazomkabili za kukiuka maadili ya utumishi wa umma kwa kuvunja Sheria ya Mwaka 1995, kifungu namba 12(e) (1).
Baada ya kusema hayo, Chenge aliinuka na kuendelea kusisitiza kuwa Baraza hilo halina mamlaka ya kuendelea kujadili shauri hilo kwa sababu kuna suala la sheria Mahakama Kuu.
“Naheshimu baraza hili ndiyo maana nimekuja mwenyewe kuwasikiliza. Ila napata tabu kujua kama wanasheria wako wa sekretarieti ya maadili wanaweza kujua tafsiri ya sheria
ya maana ya zuio la Mahakama Kuu.
“Kwa sababu nakuheshimu mheshimiwa Mwenyekiti na sina nia ya kubishana na baraza lako, nataka kutoa taarifa ya kukata rufaa na kulipeleka suala hili Mahakama Kuu iweze kutupa tafsiri ya neno zuio.
“Wanasheria wa sekretarieti wangejipima kidogo kwenda katika masijala ya Mahakama Kuu kuomba yaliyomo waweze kujiridisha kwamba amri hiyo inaruhusu kusikilizwa kwa shauri au la.
“Kama Mahakama hiyo itaona kuna umuhimu wa baraza hili kuendelea kujadili shauri hili, nipo tayari kuhojiwa, lakini ikionekana baraza hilo halina mamlaka ya sheria ya kujadili suala hili siwezi kuhojiwa.
“Ili nipate haki, ninakuomba mwenyekiti tusubiri uamuzi wa Mahakama Kuu na tafsiri ya sheria ya zuio halafu tutaendelea na vikao kama itaonekana inafaa kufanya hivyo na kama haifai, basi,”alisema Chenge.

Baada ya kusema hayo, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Hamis Msumi alikubaliana na ombi la Chenge na kumwambia kuwa sheria inamhuruhu kukata rufaa kama anaona baraza halitendi haki.
“Uko sahihi, tutakupa barua ya kupeleka Mahakama Kuu uweze kuwasilisha taarifa zako, kwa sasa, hatuwezi kujadili suala hili mpaka uamuzi wa Mahakama Kuu ukapofanyika,” alisema Jaji Msumi.
Kwa mujibu wa jaji huyo, Mahakama Kuu ni chombo muhimu kinachotoa haki kwa kila mmoja, hivyo Chenge yupo sahihi kuomba rufani kwa sababu anaamini mahakama hiyo inaweza kumsaidia zaidi kuliko baraza.
“Ni bora aende Mahakama Kuu ili tupate
historia itakayoweza kulisaidia baraza hili kufanya shughuli zake kwa umakini zaidi kwa sababu katika historia ya baraza hili, haijawahi kutokea mlalamikaji kukata rufaa ya kuomba tafsiri ya vifungu vya sheria kwenda Mahakama Kuu.
“Ni mara ya kwanza tangu kuanza kwa baraza hili kwa mlalamikaji kukata rufaa, haijawahi kutokea, lakini pia ni haki yake ya msingi kufanya hivyo,”alisema.

Alisema uamuzi huo wa Chenge utasaidia kuweka kumbukumbu nzuri kwa siku zijazo ili kama kutatokea shauri kama hilo mbele ya baraza ambalo pia liko mahakamani lijue namna ya kufanya.
Akisomewa mashtaka yake juzi, Chenge alituhumiwa na baraza hilo kukiuka maadili ya uongozi wa umma kwa kujilimbikizia mali binafsi katika kipindi cha uuzwaji wa hisa za VIP Engireering kwenda Independent Power Tanzania
Limited (IPTL).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles