27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 7, 2023

Contact us: [email protected]

Diwani Chadema adaiwa kumpiga mjamzito

DiwaniAsifiwe George na Veronica Romwald, Dar es Salaam
DIWANI wa Kata ya Saranga wilayani Kinondoni, Ephraim Kinyafu (CHADEMA) anadaiwa kumshambulia kwa mateke na fimbo, Aisha Mosses, ambaye ni mjamzito akimtuhumu kuwa ni mamluki.
Tukio hilo lilitokea jana katika Mtaa wa Saranga ambako hatua ya uandikishaji wananchi kwa ajili ya kurudia uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao awali ulivurugika, lilikuwa likiendelea.
Akizungumza na MTANZANIA shuhuda wa tukio hilo, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa mtaa huo, Majaliwa Kayombo alisema tukio hilo lilitokea mchana.
“Wananchi walikuwa wakija kujiandikisha kwa ajili ya kurudia uchaguzi kutokana na ule wa awali kuvurugika… Aisha wakati huo alikuwa amekaa chini akipumzika, Kinyafu akiwa na vijana walimvamia na kumshambulia,” alisema Kayombo.
Kayombo alisema mama huyo alipigwa kwenye kiwiko cha mkono na begani.
“Ingawa tulijitahidi kuwadhibiti na kuwasihi kuacha kumpiga mama huyo lakini waliendelea na mwishowe wakakimbia, tulimchukua na kwenda kuripoti katika Kituo cha Polisi Mbezi kwa Yusuph,” alisema.
Alisema Aisha alipatiwa fomu ya matibabu ya PF3 na kwenda kutibiwa katika zahanati ya Mbezi Mwisho pamoja na oda ya kuwatafuta watuhumiwa (RB)
MTANZANIA lilimtafuta Kinyaf kupata ufafanuzi kuhusiana na tuhuma hizo lakini alisema hana taarifa juu ya tukio hilo.
“Ndiyo mwandishi…. nimekusikia lakini binafsi sina taarifa juu ya tukio hilo unalonieleza labda nifuatilie zaidi,” alisema kabla ya kukata simu yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilus Wambura alisema taarifa hizo bado hazijamfikia na kuahidi kuzifuatilia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles