MSANII wa muziki wa hip hop nchini, Claudia Lubao ‘Chemical’, amewataka wasanii wa kike wafanye vitu vinavyoonekana vigumu kufanywa na wanawake ili wadhihirishie umma sera ya haki sawa kwa wote.
Chemical alisema mabinti wengi wanahofu ya kufanya aina hiyo ya muziki kwa sababu inaeleweka kuwa muziki ni kwa ajili ya wanaume pekee kitu ambacho si sahihi.
“Kikubwa ni kuthubutu na kufanya kile tunachokipenda bila kujali kitapokelewa kwa mtazamo gani kama mimi nafurahi kuwa msichana ninayeshindana na wavulana kwenye muziki wa hip hop na hii yote kwa sababu niliamini uwezo wangu,” alisema Chemical.