26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

CHANZO CHA MOTO NYUMBA YA ZITTO CHATAJWA

Siku moja baada ya kuungua kwa nyumba ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe Jeshi la polisi mkoani humo limesema chanzo cha moto huo ni betri za umeme wa jua kuzidiwa nguvu.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ferdinand Mtui, amesema uchunguzi wa awali umebaini moto huo ulizuka baada ya betri hizo kuzidiwa nguvu na kulipuka na kusababisha moto huo ulioteketeza mali zote zilizokuwamo ndani.

“Hata hivyo uchunguzi bado unaendelea kubaini kama kuna uzembe wowote. Lakini pia Jeshi la Polisi linawasihi wananchi kuweka vifaa vya kuzimia moto na kuchukua tahadhari na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye mfumo wa umeme pindi wanapogundua tatizo lolote watoe taarifa kwa mamlaka husika,” amesema.

Amesema eneo ilipo nyumba hiyo iliyoko Mwandiga, mkoani Kigoma ina nyumba mbili ambapo nyumba inayotumiwa na wafanyakazi wa mbunge huyo, ndiyo iliyoungua.

Pamoja na mambo mengine, Kamanda Mtui ametaja mali zilizoteketea katika tukio hilo kuwa ni pamoja na vitanda vitatu, godoro moja, seti moja ya sofa, mota ya kupandishia majibetri nne za umeme wa jua na vitu vingine vidogo ambavyo thamani yake bado haijajulikana.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles