22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

BAVICHA YAWAPIGA CHENGA POLISI KUMUOMBEA LISSU

Mkutano wa kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ulioandaliwa na Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), leo umeota mbawa baada ya polisi kuuzingira uwanja uliopangwa kufanyika maombezi hayo.

Maombi hayo, yalikuwa yafanyike katika Uwanja wa TP, Sinza Darajani jijini Dar es Salaam, yameshindwa kufanyika baada ya polisi kuimarisha ulinzi uwanjani hapo na maeneo jirani ambapo magari zaidi ya 10 mengine binafsi na askari zaidi ya 50, walitapakaa uwanjani hapo na katika Kanisa la Waadventista Wasababto (SDA), lililoko mkabala na uwanja huo.

Wakati jeshi hilo likifanikiwa kuimarisha ulinzi lilijikuta likizidiwa kete na wafuasi hao wa Chadema ambao walifika katika viwanja hivyo saa nne asubuhi kisha kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya maombi hayo.

Wakati Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi na wafuasi zaidi ya 15 wakiendelea kuelezea shughuli hiyo wakiwa wamevalia fulana zilizoandikwa ‘Pray For Lissu’ ghafla polisi waliibuka na kuwafukuza.

Katika sakata hilo wafuasi watano walitiwa mbaroni huku polisi wakiendelea kuwasaka watakaokaidi agizo la kutokufanyika kwa maombi hayo.

Hata hivyo, Katambi amesema katika maombi hayo walipanga kumuombea Lissu na Meja Jenerali Mstaafu, Vincent Mritaba ambaye naye alijeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana na kumpora Sh milioni tano.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro amesema wanaendelea kuwahoji watuhumiwa hao ili waeleze wametumwa na nani na kwa dhamira gani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,167FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles