25.3 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Changamkieni fursa za biashara Tanzania na Iran

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

WATANZANIA wametakiwa kutumia fursa za biashara, afya na nyingine zinazopatikana nchini Iran kwa ajili ya kujiendeleza na kupata ujuzi.

Hayo yamebainishwa Julai mosi na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Latifa Khamis, katika siku maalum ya Iran, katika maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara maarufu Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Amsema wametenga siku hiyo kutokana na uhusiano mzuri wa miaka 40 baina ya Tanzania na Iran, hivyo ni sehemu nzuri ya kuwekeza katika nchi hiyo.

“Tumieni maonesho haya kuzijua fursa za kibiashara zinazopatikana Iran na Tanzania kwa ujumla ili kukuza biashara na kuinua uchumi wa nchi na hakuna masharti magumu ya viza ya kusafiria nchini humo,” amesema Latifa.

Amesema bidhaa zinazozalishwa nchini humo zina ubora hata gharama zake ni nafuu nakwamba kuna haja ya kutumia fursa ya masomo hususan eneo la afya, ili nchi iweze kuzalisha madaktari bora.

“Wafanyabiashara wa na Iran ni watu wa imani hivyo ni waaminifu katika sekta mbalimbali,” amesema.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Tantrade, Profesa Ulimboka Mbamba amesema kwa kutumia siku ya Iran ni wakati wafanyabiashara kukutana na kujadiliana namna ya kuzifikia fursa zilizoko baina ya nchi hizo.

Amesema tayari Serikali imeweka mazingira bora ya biashara ili kuvutia wawekezaji katika nyanja mbalimbali.

Naye Balozi wa Iran nchini Tanzania, Hussein Behineh amesema Serikali ya Iran iko tayari kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo na kuboresha mawasiliano baina ya wafanyabiashara pande zote.

Amesema Iran ni nchi inayoongoza kwa bara la Asia katika eneo la sayansi na kukua kwa vyuo vikuu vinavyofikia 2,569 pamoja na vituo vya elimu ya juu vyenye wanafunzi wanaokadiriwa kufikia milioni nne ambapo wanafunzi 94,000 ni kutoka nje ya nchi hiyo katika nchi 129 wakisomea Taaluma mbalimbali tofauti

“Kuna maeneo mazuri kwa wanafunzi wa Watanzania kwenda kusoma kuhusu biashara wa kipindi cha miaka miwili kuanzia 2021/22 kiwango cha biashara kati ya Iran na Tanzania kiliongezeka ikilinganishwa na mwaka 2019/20,” amesema Balozi Behineh.

Amesema kwa kipindi cha 2021/22 Iran iliingiza dola milioni 95 nchini Tanzania ambazo ziliongezeka kwa asilimia 15 ikilinganishwa na miaka miwili ya 2019/20.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles