28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Chadema yahofia vyama vya siasa kufa muswada huu ukipitishwa

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam 

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar, Salum Mwalimu, amesema muswada mpya wa sheria ya vyama vya siasa uliosomwa bungeni Novemba 16 mwaka huu, ukipitishwa na kuwa sheria kamili utaenda kuua na kuvuruga vyama vya siasa nchini.

Ameyasema hayo leo Jumapili Desemba 9, katika mkutano wa vyama vya siasa 15 na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati vyama hivyo vikiwasilisha tamko lao la kupinga muswada huo.

Amesema vyama vya siasa vimekuwa vikivurugwa kwa muda mrefu ikiwamo kukamatwa na kupigwa na kuingiliwa maisha yao binafsi ila sasa sheria inakuja ili kuwanyamazisha kabisa wanasiasa nchini na hii ni kuvunja misingi ya waasisi wa taifa ambao walitaka kuwepo na siasa za ustarabu zenye kujenga ustawi wa jamii.

” Kifungu kipya namba 5 (a) cha muswada huo kinampa kibali msajili wa vyama vya siasa kuomba taarifa za vyama, hata tukitaka kutoa mafunzo kwa wanachama wetu lazima tuseme yanahusu nini na yanafadhiliwa na nani ni lazima tumwambie na yeye ndiyo atoe kibali.

“Dhana hii sidhani kama inakubaliwa sehemu yoyote ile, yaani msajili akiagiza chama fulani kifanye marekebisho ya katiba zao na wasipobadilisha ndani ya miezi sita wanafutiwa usajili hii siyo haki mtu mwingine kuamua mambo ya mtu mwingine, ” amesema Mwalimu.

Aidha Mwalimu amesema sheria hiyo mpya inampa msajili kibali cha kumfuta uanachama mwanachama yeyote jambo ambalo wanaona kama limewalenga hasa viongozi wakubwa kwani ni ngumu msajili kuwajua hadi wanachama wa mikoani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles