26.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 6, 2021

Nikki wa Pili amvisha pete mchumba wake

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam


Msanii wa Hip Hop nchini Nickson Simon maarufu Nikki wa Pili amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake aliyemtaja kwa jina moja la Joan jambo linalodhihirisha kuwa ndoa ya wawili hao imekaribia.

Leo Jumapili Disemba 9, Nikki ametumia ukurasa wake wa Instagram kutuma ujumbe na picha kuthibitisha tukio hilo akiambatanisha na picha inayomuonesha amepiga goti akimvisha pete mpenzi wake huyo.

“Malkia mwenye moyo wangu, nuru ya uzuri wako imulike njia ya maisha yetu, nakupenda sana na ahadi ya kwanza nimetimiza,” ameandika Nikki akimweleza mpenzi wake huyo.

Aidha wasanii wenzake waliohudhuria sherehe hiyo akiwemo kaka yake, John Simoni maarufu Joh Makini, Abdulaziz Chande maa (Dogo Janja), Juma Khaleed (Juma Jux) na Isack Waziri (Lord Eyez). Aidha mashabiki na wasanii mbalimbali wametoa maoni yao wakiwapongeza wawili hao kwa tukio hilo kubwa.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,340FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles