Diamond aanguka jukwaani, aumia mkono

0
1845

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz, ameanguka jukwaani leo Jumapili Desemba 9,  wakati akitumbuiza jukwaani katika Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Sumbawanga mkoani Rukwa katika Tamasha la Wasafi (Wasafi Festival).

Kipande cha video kilichosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kinamuonesha Diamond akitumbuiza sambamba na msanii mwenzie kutoka Wasafi, Raymond Mwakyusa maarufu Rayvanny, wakiimba na kucheza wimbo wa Zilipendwa ndipo jukwaa lilishindwa kuhimili mikiki ya wasanii waliokuwa wakiruka ruka na kuvunjika na kisha kuangukia ndani ya jukwaa hilo la kutengenezwa.

Katika ukurasa wake wa Instagram leo, Diamond ameandika ameumia mkono katika tukio hilo na tayari amepaka dawa ya ‘spirit’.

Tamasha hilo ambalo lilipangwa kufanyika mkoani humo jana usiku lakini lilihairishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kupangwa kufanyika leo mchana.

Hili ni tukio kubwa la pili katika mfululizo wa tamasha hilo ambalo msanii huyo hakutegemea limtokee ambapo akiwa mkoani Mtwara aliibiwa mkufu wenye thamani ya Sh milioni 40.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here