30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Chadema waunda safu mpya Kigoma

Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Na Editha Karlo, Kigoma

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Kigoma, kimefanya uchaguzi na kuchagua viongozi wa chama hicho wa mkoa na wilaya.

Mkurugenzi Mkuu wa Oganaizesheni na Usimamizi katika chama hicho, Benson Kigaila ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo, alisema ulifanyika kuziba mapengo yaliyoachwa wazi baada ya viongozi kujiuzulu.

Kigaila aliwataja viongozi waliochaguliwa ambao watashika madaraka hayo hadi uchaguzi utakapofanyika kwa mujibu wa katiba Agosti 30 mwaka huu kuwa ni Ally Kisala ambaye ni Diwani wa Mwandiga aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Chadema Mkoa wa Kigoma.

Aliyechaguliwa kuwa Katibu wa Mkoa alimtaja kuwa ni Shabaan Madebe wakati nafasi ya Mratibu wa Baraza la Wanawake wa mkoa huo (BAWACHA), ilichukuliwa na Vestina Luhihi.

Omary Gindi alichaguliwa kuwa Mratibu wa Baraza la Vijana mkoani humo wakati Jeremia Misigara alichaguliwa kuwa Mratibu wa Baraza la Wazee.

“Tumefanya pia uchaguzi wa viongozi wa Jimbo la Kigoma mjini ambako Mwenyekiti aliyechaguliwa ni Khalfani Bona na Katibu wake ni Frank Luhasha.

“Katibu Mwenezi ni Idd Ngesha na Mratibu wa Wazee ni Yassin Mapigo wakati Amfua Athumani ni Mratibu wa BAVICHA,” alisema Kigaila.

Kwa mujibu wa Kigaila, viongozi hao waliochaguliwa wanatakiwa kuanza kazi mara moja na jukumu lao kuu ni kukifanya Chadema Mkoa wa Kigoma kizidi kusonga mbele.

“Tumeshawahoji hawa makamanda mmoja mmoja kama kazi hiyo tuliyowapa ya uongozi wataifanya kwa moyo wao wa kujitolea bila ya malalamiko nao wametuahidi hawatatuangusha.

“Pia nimewaambia wafanye kazi kwa moyo wa kujitolea na siyo kuwa ndani ya chama nusu nusu yaani mguu mmoja ndani na mwingine nje,” alisema Kigaila.

Akizungumzia chama kipya cha ACT, alisema hakijaleta madhara mkoani Kigoma dhidi ya Chadema.

Mwenyekiti mpya wa Mkoa Kigoma, Ally Kisala, alisema pamoja na mkoa huo kuwa na changamoto nyingi za siasa, atashirikiana na viongozi wenzake kukiimarisha chama chao.

- Advertisement -

Related Articles

4 COMMENTS

  1. MAKAMANDA TUSONGE MBELE PASIPO KUKATA TAMAA WAKATI WENZETU WANACHOKA NA SAFARI NA WAKINUNULIWA NA ccm WAKITHANI WANAKIDHOFISHA CHAMA SISI TUNAZIDI KUWA IMARA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015 “KWA SABABU TULIANZA NA MUNGU PIA TUTAMALIZA NA MUNGU .PEOPLE’S POWER!

  2. MAKAMANDA TUSONGE MBELE PASIPO KUKATA TAMAA WAKATI WENZETU WANACHOKA NA SAFARI NA WAKINUNULIWA NA ccm WAKITHANI WANAKIDHOFISHA CHAMA SISI TUNAZIDI KUWA IMARA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015 “KWA SABABU TULIANZA NA MUNGU PIA TUTAMALIZA NA MUNGU” .PEOPLE’S POWER!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles