27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Chadema wapongezwa uteuzi wa Dk. Mashinji

MtatiroCHRISTINA GAULUHANGA NA HERIETH FAUSTINE , DAR ES SALAAM

BAADHI ya wanasiasa na wananchi wa kada mbalimbali wamepongeza hatua ya Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa kupitisha uteuzi wa Dk. Vicent Mashinji, kuwa katibu mkuu wa chama hicho.

Wakizungumza na  MTANZANIA kwa nyakati tofauti jana, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro, alisema uteuzi wa Dk. Mashinji umekuwa wa siri na umekiletea chama hicho heshima ya kipekee.

Alisema hatua ya uteuzi wa Dk. Mashinji, ambaye ameteuliwa kushika nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Dk. Willbrod Slaa,  umekiletea heshima kuingia katika historia kwa chama hicho.

Dk. Slaa, alitangaza kujiengua  katika nafasi hiyo na kujiweka kanda na siasa na kwa sasa anaishi ughaibuni nchini Canada.

“Vyama vya upinzani katika hili la Dk. Mashinji tumejifunza kuwa wapinzani wana uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi muhimu kwa siri kuliko chama tawala cha CCM na serikali yake,” alisema Mtatiro.

Alisema watu mbalimbali walikuwa wanashinda kwenye mitandao wakitabiri jina la Katibu Mkuu huku wakipambanua weledi na uwezo wa katibu wanayemtaka lakini cha ajabu wote walikosea.

“Kila mmoja aliyetabiri alikosea na huenda wote waliokosea kama wangewekeana ahadi huenda wangemlipa fedha nyingi na angeweza kuwa bilionea Mwenyekiti wa chama hicho,  Freeman Mbowe kwakuwa wameliwa,”alisema Mtatiro.

Mtatiro alisema kwa wanaomfahamu Dk. Mashinji ni mtu makini ana uwezo wa kukisaidia chama hicho kwa kuwa anafahamu siasa za kisasa na ataipeleka Chadema katika hatua za juu zaidi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Sanaa na Uhamasishaji Ofisi ya Katibu Mkuu (Chadema), Fullgency Mapunda, alisema amefarijika na uteuzi na Baraza Kuu la Taifa kumchagua kiongozi makini na anaamini atafanya mabadiliko makubwa yatakayosaidia kukivusha chama hicho.

“Kuchaguliwa kwa Dk. Mashinji kamati Kuu  kwa kushirikiana na mwenyekiti wa chama hawakufanya makosa kwani wana amini mipango iliyokuwa imekwama inakwenda kutekelezwa,”alisema Mapunda.

Naye, Ommy Herman alisema yeye kama mwanaharakati hawezi kuacha kusifia uteuzi huo kwa kuwa imefuta tetesi za watu waliodai aliyekuwa Waziri Mkuu, Fredrick Sumaye ndiye angekuwa Katibu Mkuu.

Kwa upande wake Chriss Zephania, alisema hana shaka na uteuzi wa Dk. Mashinji, kwa kuwa anaamini kamati tendaji haikukurupuka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles